-
Version
-
Download
1 -
File Size
5.11 MB -
File Count
1 -
Create Date
November 6, 2023 -
Last Updated
November 6, 2023
Sera ya Muundo Mbadala wa Mifumo ya Haki
Tarehe 4 Machi 2016 aliyekuwa Jaji Mkuu, Mhe. (Dkt) Willy Mutunga aliteua Jopokazi la
Mifumo Mbadala ya Haki kutathmini Mifumo mbalimbali ya Kitamaduni, Isiyo Rasmi na Mingineyo
Inayotumiwa Kupata Haki Nchini Kenya (Mifumo Mbadala ya Haki) na kubuni sera ya kitaifa kuhusu
Upatikanaji wa Haki. Kwa zaidi ya miaka minne, Jopokazi, ambalo muda wake uliongezwa hadi Aprili
2020 na Jaji Mkuu Mhe. David Maraga, lilifanya utafiti, kuenda nyanjani, na mashauriano ya kina
na washikadau. Kazi ya Jopokazi hilo ilisababisha kuwepo kwa rasimu ya sera – Haki kama Uhuru:
Mifumo ya Kitamaduni, Isiyo Rasmi na Mingineyo ya Utatuzi wa Mizozo nchini Kenya – ambayo
hutumika kama mpango wa utekelezaji na uingiliaji kati kuanzisha Mifumo Mbadala ya Haki (AJS).
Sera hii ya Muundo wa AJS (Sera) ni matokeo ya kazi ya Jopokazi.
Sera hiyo inachukulia AJS kuwa kipengele muhimu cha kupata haki na lengo lake kuu ni kutekeleza
Ibara ya 159(2)(c), ambayo inaidhinisha Idara ya Mahakama, kama chombo cha Serikali, ili kukuza
AJS. Katika ngazi ya kimataifa, AJS ni mfumo wa kuhakikisha upatikanaji wa haki chini ya Lengo la
16 la Maendeleo Endelevu la Umoja wa Mataifa, ambalo linawajibisha viongozi wake ‘kukuza jamii
zenye amani na umoja kwa ajili ya maendeleo endelevu, kuhakikisha upatikanaji wa haki kwa wote na
kujenga taasisi zenye ufanisi, uwajibikaji na shirikishi katika ngazi zote’.